Alhamisi 5 Februari 2026 - 00:30
Mapinduzi ya Kiislamu ni Kuzaliwa upya Ustaarabu wa Kimataifa wa Mahdawiya/ Naibu wa Imam wa Zama (a.j) ndie Nahodha wa Mapinduzi

Hawza/ Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum amesisitiza kuwa; Mapinduzi ya Kiislamu yaliundwa juu ya misingi ya Ghadir, Ashura na Subira ya Kungoja (Intidhār), na kwa msingi wa uwakala wa jumla wa Imam wa Zama (a.j) katika mfumo wa Wilayat al-Faqih.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Abbas Kaabi, Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum, katika mahojiano na Shirika la Habari la Hawza, alisema kuwa; Mapinduzi ya Kiislamu ni urejeshaji wa mwenendo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa kuzingatia mafundisho ya Ahlul Bayt (a.s) katika zama za sasa. Alisisitiza kuwa; mapinduzi haya yana uwezo wa ustaarabu wa kimataifa na kimaumbile (kifitra), na walengwa wake ni wanadamu wote wanaokubali kuongozwa.

Aliongeza kuwa: Utekelezaji wa ustaarabu mpya wa Kiislamu unapatikana kupitia miongozo na ufafanuzi wa uongozi wa Kimungu, pamoja na ijtihadi asilia inayolingana na mahitaji ya wakati na uendeshaji wa masuala ya binadamu wa leo. Kwa hakika, Mapinduzi haya yamejengwa juu ya msingi wa Ghadir, yamechota msukumo kutoka katika utamaduni wa Ashura, na kwa upande mwingine yamejikita katika utamaduni wa kusubiri kudhihiri. Kwa njia hiyo, yameunda mazingira ya kuleta mabadiliko ya msingi katika muundo, maudhui na uongozi wa dunia kwa misingi ya Tawhidi, uadilifu na heshima ya mwanadamu.

Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi (Majlisi Khabregan), akirejea mafundisho ya Mahdawiyya, alisema: Katika mafundisho haya, uongozi wa Kimungu hushika hatamu za kusimamia mambo ya binadamu na huijenga upya jamii kwa misingi ya imani, Tawhidi na matendo mema, ambayo yamesimama juu ya kupambana na udikteta, ukoloni na kufufua utambulisho wa asili wa mwanadamu.

Mapinduzi ya Kiislamu ni Kiwanja cha Kuandaa Mapinduzi ya Kimataifa ya Imam Mahdi (a.j)

Ayatullah Kaabi aliendelea kwa kusema kuwa; Mapinduzi ya Kiislamu ni kiwanja cha maandalizi ya Mapinduzi ya Kimataifa ya Hadrat Baqiyyatullah al-A‘dham (a.j), na akasema: Mapinduzi haya yaliundwa kwa msingi wa Wilayat al-Faqih kama uwakala wa jumla wa Imam wa Zama (a.j).

Akifafanua aina mbili za Uimamu, alisema: Tuna aina mbili za uimamu: uimamu wa asili (bil-asalah), ambao ni uimamu wa Imam wa Zama (a.j), na uimamu wa uwakala (bil-niyabah), ambao ni Wilayat ya Walii wa Fiqhi. Mapinduzi ya Kiislamu yalijengwa juu ya mafundisho ya Uislamu na ijtihadi halisi, uelewa na utambuzi wa mahitaji ya wakati, miongozo ya Walii wa Fiqih, uhamasishaji wa uwezo wa wasomi wa hawza na vyuo vikuu, pamoja na ushiriki wa wananchi katika uwanja wa mapambano.

Mjumbe huyo wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi huku akigusia nafasi ya subira na muqawama katika ushindi wa Mapinduzi, aliongeza kuwa: Mapinduzi haya yalisimama imara kwa subira na muqawama dhidi ya changamoto na njama mbalimbali, na yakavuka hatua ngumu kwa mafanikio. Leo pia, kwa misingi ya jihadi, muqawama na kunufaika na hazina ya kimkakati ya Mapinduzi ya Kiislamu — ambayo ni uwepo wa wananchi katika uwanja — yanaendelea kusonga mbele katika maendeleo yake.

Fikra ya Mapinduzi ya Kiislamu Inaendelea Kusonga Mbele

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum alisema kuwa: Mapinduzi ya Kiislamu yanaendeleza malengo yake makuu kwa mujibu wa mafundisho ya Kimahdi, na akaongeza: Tunajivunia Mapinduzi ya Kiislamu, na ni neema ya kipekee sana ambayo imevunja vizuizi na kuufikisha ujumbe wa Mapinduzi na wa taifa la Iran katika kiwango cha kimataifa.

Akichambua mabadiliko katika mfumo wa kimataifa, Ayatullah Kaabi alisema: Kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, dunia ilikuwa imegawanyika katika nguzo mbili: Mashariki na Magharibi. Leo pia dunia ina nguzo mbili; nguzo ya kwanza ni mfumo wa utawala wa kidhalimu unaoelekea kudhoofika, unaojengwa juu ya demokrasia ya kiliberali, na nguzo ya pili ni nguzo inayosonga mbele kwa misingi ya fikra ya Mapinduzi ya Kiislamu. Nguzo hii ya pili ni nguzo ya Wilaya ya Muhammad na Aali Muhammad (s.a.ww).

Ayatullah Kaabi, mwishoni, akirejea subira ya kungojea faraja (intidhār al-faraj), alisema: Sisi tuko katika matarajio ya kuonekana kwa jua na kutimia kwa Wilaya tukufu wa Hadrat Baqiyyatullah al-A‘dham (a.j). Mapinduzi ya Kiislamu ni kiwanja cha kuandaa kudhihiri huku na kutimiza malengo ya kimataifa ya Uislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha